March 14, 2015


FULL TIME:
GOOOOOOOO Dk 90+3 Okwi anaifungia Simba umbali wa mita 25 baada ya kugeuka na kupiga shuti kali linaloingia kwenye engo la lango.

MWAMUZI ANAONYESHA Dakika 5 za nyongeza

Dk 90, Simba tena wanafanya shambulizi kali, Ndemla anapiga shuti kali, litatoka (kipa wa Mtibwa analala chini kuwa ameumia, ikionekana anataka kupunguza presha ya mashambulizi).
Dk 85, Okwi tena anapiga tena shuti lakini mabeki wa Mtibwa wanaokoa
Dk 80, Okwi tena anaingia eneo la hatari na kuangushwa. Faulo inapigwa na Singano, lakini inagongwa na kuwa kona.



Dk 75 Okwi anawatoka mabeki tena na kupiga krosi safi lakini kipa anaokoa na kugongana na Maguri (saa wanatibiwa).

Dk 69 Okwi anawatoka mabeki wawili wa Mtibwa na kupiga krosi safi kwa Maguri ambaye anaonekana kutokuwa makini na kupaisha lango likiwa halina mwenyewe.

Dk 65 Mohammed Mkopi anaingia kuchukua nafasi ya Ame Ally kwa upande wa Mtibwa Sugar
Dk 60, Ivo anadaka kama nyani shuti kali la Mgosi

Dk 58, Juuko anaruka na kuukosa mpira akiwa hatua nne kutoka lango la Mtibwa baada ya krosi safi ya KEssy.
Dk 53, Mkude anaondosha hatari baada ya Mtibwa kugongeana vizuri katika eneo la Simba
Dk 48, Mohammed Hussein anafanya kazi ya ziada kuokoa krosi ya Mgosi na kuwa kona ambayo haina matunda.


Dk 46, mwamuzi anatoa kadi ya njano kwa Mgosi baada ya kuushika mpira
Dk 46, Simba wanamtoa Simon Sserunkuma na nafasi yake kuchukuliwa na Ramadhani Singano 'Messi'
MAPUMZIKO
Dk 45, Okwi anawatoka mabeki wa Mtibwa na kutoa pasi safi kwa Maguri anapiga na kipa Said Mohammed anaokoa vizuri kabisa.

Dk 44 Mgosi anapiga shuti kali mita 30, lakini Ivo Mapunda anafanya kazi ya ziada kupangua na kuwa kona.
Dk 32 hadi 39; mechi inaonekana kupooza na zaidi mpira unachezwa katikati ya uwanja. Dakika moja inatumika kumtibu Ame Ally aliyegongana na Juuko Murshid.


Dk 30, Mtibwa Sugar wanaonekana kuinuka sasa, wanajitahidi kufika katika lango la Simba
Dk 26, Mussa Hassan Mgosi anamjaribu Ivo Mapunda kwa shuti kali, lakini mpira unapaaa juu.


Dk 23, Okwi anapiga shuti kali baada ya kuwatoka mabeki wa Mtibwa lakini mpira unapaaa.
Dk 15 hadi 20, Simba wanaonekana kuamka na mara mbili Hassan Kessy napiga krosi safi kabisa lakini Mtibwa wanaokoa.


Dk 2 hadi 11 Kipindi cha kwanza kinaonekana kutokuwa na msisimko sana kwa mpira kuchezwa zaidi katikati ya uwanja.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic