![]() |
| MAFTAH 'PELE WA MWANZA' (KULIA) AKIWA NA LUNYAMILA WAKATI WA KUUAGA MWILI WA KOCHA MARSH JIJINI MWANZA. |
Wanasoka wa zamani wa Simba na Yanga, Juma
Amir Maftah 'Pele wa Mwanza' na Edibily Lunyamila wameeleza kuhuzinishwa kwao na msiba wa Kocha
Sylvester Marsh.
Marsh alifariki jijini Dar es Salaam, Jumamosi iliyopita na kusafirishwa na kuzikwa jijini Mwanza, jana.
Lunyamila aliyesafiri hadi Mwanza, amesema
Marsh alikuwa ni sehemu ya makocha bora wanaochipukia kufikia kuitwa mahiri na
tegemeo la soka la vijana, lakini sasa hatukonaye.
“Mungu anachukua uamuzi usiokosolewa. Lakini
Marsh alikuwa muhimu kila mtu anajua. Mimi sikupenda namna alivyosaidiwa na
hasa na wahusika wakuu kama TFF. Lakini yote tumuachie Mungu.
“Kikubwa ni watu kuiga mfano wake kwa kuwajali zaidi vijana ambao aliwapa kipaumbele kwa kiasi kikubwa,” alisema.
Kwa upande wa Maftah aliyewahi kung’ara
akiwa Pamba, Simba na Taifa Stars, alisema Marsh alikuwa tegemeo la maisha ya
soka na hasa kwa vijana.
“Alikuwa akiibua vijana, makocha wengi
wamefuata mfano wake. Kwetu hapa Mwanza kila mtu anaujua mchango wake.
“Lakini amevuka zaidi hadi kuwa tegemeo la
nchini. Vizuri tumuenzi kwa ubora wa kazi zake,” alisema Pele.








0 COMMENTS:
Post a Comment