Mashabiki wa
FC Platinum ya Zimbabwe wametamba hakuna wa kuizuia timu yao katika ukanda wa
Afrika Mashariki.
Mashabiki
hao wametamba katika mitandao mbalimbali kuwa FC Platinum itaiadhibu Yanga kama
ilivyofanya kwa Sofapaka ya Kenya.
Baadhi ya mashabiki tayari wako jijini Dar es Salaam na wametamba katika mitandao ya kijamii hasa Twitter na Facebook kwamba wataondoka na ushindi.
Platinums
iko jijini Dar es Salaam, tayari kuivaa Yanga katika mechi ya kwanza ya Kombe
la Shirikisho.
Kabla ya
kukutana na Yanga, FC Platinum iliing’oa Sofapaka ya Kenya kwa kuishinda
nyumbani na ugenini.
Mashabiki
hao wanaamini, ndicho kitakachowakuta Yanga waliong’oa BDF XI ya Botswana.
Hata hivyo,
Yanga ambayo mechi yake ya mwisho ililala kwa bao 1-0 dhidi ya Simba,
imesisitiza itafanya vema katika mechi ya leo.
Sio kosa lao, walikuwa hawajui moto wa Yanga. Bhahahahahahahaaaaa
ReplyDelete