March 15, 2015


MDAU WA SOKA NCHINI, ABDULFATAH SALEH AKISHIRIKI KATIKA KUMUAGA KOCHA MARSH, LEO.

Wadau mbalimbali wa mchezo wa soka wakiwemo ndugu jamaa na marafiki wamejitokeza leo kumuaga Kocha Sylvestre Marsh katika safari yake ya mwisho.


Marsh amefariki dunia jana na kuagwa leo kwenye Hospitali ya Taifa ya Muhimbili jijini Dar es Salaam.

Wadau mbalimbali wakiwemo wachezaji wa zamani, wale wanaoendelea kucheza. Waliowahi kufanya naye kazi na wengine wengi walikuwa katika eneo hilo kwa ajili ya kumuaga.

Baada kuagwa, taarifa zilieleza kuwa mwili huo utaanza safari ya basi kwenda jijini Mwanza ambako atazikwa.

BURIANI KOCHA MARSH, SAFARI YAKO NDIYO NJIA YA SISI SOTE.

ALLY YANGA ALIKUWEPO...







0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic