March 3, 2015


Aliyekuwa Kocha wa Simba, Patrick Phiri amesema angependa suala la mshambuliaji Amissi Tambwe asiangushiwe yeye.

Simba ilimuacha Tambwe, Yanga ilitumi mwanya huo kuokota 'dodo' na sasa amekuwa akiwafungia mabao jambo linaloonyesha kuwakera mashabiki na wanachama wa Simba.

Akizungumza kutoka nchini Zambia, Phiri amesema waandishi kadhaa kutoka Tanzania wamekuwa wakimpigia kumuuliza kuhusu hilo, jambo ambalo linamshangaza.

“Sipendi kuanzisha malumbano na watu wa Simba, wao wanajua na kuhusu Tambwe mimi sikuwahi kusema aachwe.

“Inawezekana kuna watu walifanya ujanja huo ili aachwe na wakamueleza vingine Rais Aveva kuwa mimi ndiye nilisema.

“Tambwe ni mchezaji aliyekuwa amefunga mabao mengi zaidi msimu mmoja nyuma. Hata kama angekuwa hafanyi vizuri ningependa kumpa msimu mmoja ili nijaribu kumrekebisha, lakini si kumuacha,” alisema Phiri.

“Waambie Simba wanapaswa kuwa watulivu katika wakati huu badala ya kuongeza malumbano,” aliongeza.
Hivi karibu, Rais wa Simba, Evans Aveva alisema Phiri aliwaingiza mkenge kwa kusema Tambwe aachwe.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic