March 3, 2015


Mpenzi wa winga Adam Johnson amesisitiza atamuunga mkono mpenzi wake katika kesi ya inayomkabili ya kutuhumiwa kufanya ngono na msichana mwenye umri wa miaka 15.


Johnson anayekipiga Sunderland amekamatwa juzi na tayari Sunderland imetangaza kumsimamisha kutokana na suala hilo.

Mama mzazi wa mpenzi wake amesema mwanaye Stacey Flounders atamuunga mkono winga huyo kwa kuwa anaamini hana hatia.

Stacey Flounders anatokea katika familia yenye kipato cha juu na ahadi hiyo huenda ikampa nguvu Johnson.

Winga huyo alitua Sunderland kwa kitita cha pauni milioni 10million mwaka 2012.


Polisi walikwenda kumkamata katika jumba lake la kifahari lenye thamani ya pauni milioni 1.8.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic