Timu ya
Taifa ya Tanzania ya soka la ufukweni (Beach Soccer) inatarajiwa kucheza na
timu ya Taifa ya Misri siku ya ijumaa majira ya saa 10 kamili jioni, mchezo
utakofanyika katika klabu ya Escape 1 Msasani jijini Dar es Salaam.
Kikosi cha
timu ya Taifa ya Tanzania kinaendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo huo,
ambapo kwa takribani wiki mbili kipo kambini Bamba Beach wakijifua kwa mchezo
huo.
Tanzania
ilifuzu hatua ya pili baada ya kuiondoa timu ya Taifa ya Kenya kwa jumla ya
mabao 12 -9, na endapo itafanikiwa kuwaota Misri, itafuzu moja kwa moja kucheza
Fainali za soka la Ufukweni zitakazofanyika Visiwa vya Shelisheli mwezi April
mwaka huu.
Waamuzi wa
mchezo huo ni Eid Haitham Eid Hassan (Sudan), mwamuzi msaidzi wa kwanza
Abaker Mohamed Bilal (Sudan), mwamuzi msaidizi wa pili Abdalla Hassain
Hassaballa, mtunza muda (time-keeper) Boubaker Bessem (Tunisia) wakati kamisaa
wa mchezo huo ni Khiba Herbert Mohoanyane kutoka Lesotho.
Nayo timu ya
Taifa ya Misri inatarajiwa kuwasili Dar es salaam kesho (jumatano) mchana,
ambapo itafikia katika hoteli ya Double Tree by Hilton iliyopo Masaki, huku
waamuzi wa mchezo huo wakitarajiwa pia kuwasili kesho na kufikia katika hotel
ya Protea Oysterbay.
Aidha siku
ya alhamis makocha wa timu zote wataongea na vyombo vya habari katika ukumbi wa
mikutano wa TFF uliopo Karume kuanzia majira ya saa 5 kamili asubuhi.
Mchezo wa
marudiano unatarajiwa kufanyika wiki ijayo nchini Misri kati ya Machi 20,21 na
22 mwaka huu.
Kwa niaba
ya familia ya mpira wa miguu , Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF),
inaitakia kila la kheri na ushindi timu ya Taifa ya soka la ufukweni (Beach
Soccer) katika huo dhidi ya Misri.
Wakati huo
huo michezo miwili ya Ligi Kuu ya Vodacom iliyokuwa iichezwe kesho
(jumatano) kati ya JKT Ruvu dhidi ya Young Africans katika uwanja wa
Taifa, na Mgambo Shooting dhidi ya Azam FC uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga
imeahirishwa na sasa mechi hizo zitapangiwa tarehe nyingine.
0 COMMENTS:
Post a Comment