Suala la muonekano mpya wa kipa wa Simba, Ivo
Mapunda akiwa na ndevu zenye rangi limezua gumzo nchini Kenya.
Baadhi ya mitandao ya kijamii hasa kwenye
Twitter na Facebook, mashabiki wa soka nchini Kenya wamekuwa wakijadili ubora
wa kipa huyo wa zamani wa Gor Mahia ambako alipata umaarufu mkubwa.
Mashabiki hao wamesema Ivo yuko katika kiwango
bora kabisa, lakini wengine wamekuwa wakisisitiza kwamba kipa huyo aliwatisha
washambuliaji Yanga kwa kutumia ndevu zake wakati timu hiyo iliposhinda kwa bao
1-0.
Ivo aling’ara akiwa katika lango siku hiyo,
ilikuwa pia ni siku ya kwanza kuonekana akiwa na ndevu zenye rangi.
Aliokoa hatari kadhaa, yakiwemo mashuti mawili
ya Mrisho Ngassa na Hussein Javu huku wengi wakiamini mipira hiyo ilikuwa
inatinga wavuni.







0 COMMENTS:
Post a Comment