Uongozi wa Yanga, umeendelea kisisitiza
utapeleka kikosi chake uwanjani kesho kwa ajili ya mechi dhidi ya Ruvu JKT.
Yanga imelalama kwamba Bodi ya Ligi
imeahirisha mechi hiyo bila kukaa ikazungumza nao halafu ikaipeleka mbele hadi
Machi 11 ikiwa ni siku tatu tu kabla ya kuivaa FC Platinum ya Zimbabwe.
Akizumgumza na SALEHJEMBE, Msemaji wa Yanga,
Jerry Muro amesema watapeleka timu uwanjani na kama mechi haitakuwepo, nao
hawatapeleka timu Machi 11.
“Bodi ya ligi inapaswa kuwa wazi kuhusiana
na mabadiliko, sisi tuko tayari kucheza kesho. Lakini si Machi 11.
“Angalia siku tatu mbele tuna mechi ya
kimataifa, TFF inataka tucheze mechi ya ligi. Kwa nini tusicheze kesho halafu
baada ya siku tatu tucheze na Simba.
0 COMMENTS:
Post a Comment