Timu za Ujenzi Rukwa na
Volcano FC ya Morogoro zimeshushwa madaraja mawili hadi ligi za wilaya baada ya
kushindwa kufika uwanjani kwenye mechi zao za Ligi Daraja la Pili (SDL).
Uamuzi huo umefanya na
Kamati ya Mashindano ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) iliyokutana
jana jijini Dar es Salaam kupitia ripoti za matukio mbalimbali ya ligi hiyo.
Ujenzi Rukwa ilishindwa
kwenda Kigoma kuikabili Mvuvumwa FC ya huko wakati Volcano FC haikutokea kwenye
Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya ambapo ilitakiwa kucheza na Wenda
FC.
Uamuzi wa Kamati ya
Mashindano umefanywa kwa kuzingatia Kanuni ya 27 ya SDL ambapo mbali ya
kushushwa madaraja mawili, lakini pia timu hizo zimepigwa faini ya sh. milioni
moja kila moja. Vilevile matokeo yote ya mechi zao kwenye Ligi hiyo yamefutwa.
Nayo Singida United
imepewa ushindi wa pointi tatu na mabao matatu baada ya Ujenzi Rukwa kubainika
kumchezesha mchezaji asiyestahili (non qualified) kwenye mechi iliofanyika
Februari 8 mwaka huu kwenye Uwanja wa Mandela mjini Sumbawanga na timu hizo
kutoka sare ya bao 1-1.
Mchezaji Emmanuel Elias
Mseja wa Mbao FC amepigwa faini ya Sh 100,000 na kufungiwa mechi tatu baada ya
kukojoa uwanjani kwenye mechi dhidi ya AFC iliyochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya
Sheikh Kaluta Amri Abeid jijini Arusha.
Pia viongozi wa Mbao FC,
Abdallah Chuma (Daktari) na Meneja Yasin Abdul wamefungiwa miezi sita na faini
ya Sh 100,000 kila mmoja kwa kumtukana na kumtishia maisha Kamishna wa mechi
hiyo.
Nayo klabu ya AFC
imepigwa faini ya Sh 300,000 kutokana na washabiki wake kuifanyia vurugu timu
ya Bulyanhulu FC kwenye mechi yao iliyofanyika Februari 7 mwaka huu Uwanja wa
Kumbukumbu ya Sheikh Kaluta Amri Abeid na kumalizika kwa sare ya bao 1-1.
Timu ya Magereza Iringa
imepigwa faini ya jumla ya Sh 200,000 kwa kuchelewa kufika kwenye kikao cha
maandalizi ya mechi (pre match meeting), na uwanjani kwenye mchezo wao na
Njombe Mji uliochezwa Februari 21 mwaka huu.
Naye mchezaji wa timu
Amasha Mlowasa amefungiwa mechi tatu na faini ya Sh 100,000 kwa kumtukana
mchezaji mwenzake kwenye mechi hiyo.
0 COMMENTS:
Post a Comment