April 13, 2015


Baada ya kukaa nje ya kikosi kwa muda na kukosa mechi kadhaa za Simba, kiungo tegemeo wa timu hiyo, Jonas Mkude, anatarajia kurejea rasmi kuungana na timu yake hiyo leo Jumatatu kwa ajili ya kujiwinda na mchezo wao wa Aprili 18 dhidi ya Mbeya City.


Mkude alilazimika kuukosa mchezo wao dhidi ya Kagera Sugar na ile ya kirafiki ukiwemo wa Toto African waliyoshinda kwa mabao 3-0 hivi karibuni kutokana na kufiwa na baba yake mzazi, Gerald Jonas Mkude.

Baada ya kukamilika kwa taratibu za mazishi, uongozi wa Simba ulimpa Mkude muda wa wiki moja kupumzika kutokana na msiba huo kisha baada ya hapo arejee kazini na kuendelea na majukumu ya kuitetea timu hiyo.

Mkude amesema kwamba kwa sasa yuko poa na anaweza kujiunga na wenzake kwa ajili ya kuendelea kupambana kama ilivyo kawaida.

“Tayari muda wangu wa kupumzika umeisha na sasa niko poa kabisa kurejea kwenye timu na kuanza mazoezi kama kawaida kwa ajili ya kumalizia mechi zilizobaki, kesho (leo) ndiyo nitajumuika rasmi na kikosi katika maozezi ya kitimu,” alisema Mkude. 



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic