April 17, 2015

Baada ya kutua nchini tayari kuivaa Yanga, Etoile du Sahel wametengeneza utawala wao jijini Dar es Salaam.


Kikosi hicho kilichotua nchini usiku wa maneno, tokea Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) ilikuwa ni vituko tu.

Waarabu hao hawakutaka kuzungumza na waandishi, hawakutaka maelekezo ya wageni wao Yanga ambao waliwakilishwa na Jerry Muro aliyefika uwanja wa ndege.
Kila kitu wakitaka kufanya wanavyofanya wao na utaratibu waliojipangia.
Mwisho wakaondoka uwanjani hapo na msafara wa magari takribani saba, kwenda kujichimbia katika hoteli ya Ledger Bahari Beach iliyo Kunduchi jijini Dar es Salaam.
Leo mchana, wanatarajia kufanya mazoezi yao ya kwanza na mwisho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.




0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic