April 17, 2015

MARSH (KULIA) WAKATI WA UHAI WAKE AKIWA NA BOSI WAKE, KIM POULSEN. 

Katika hali ya kushangaza, ndugu wa marehemu Sylvestre Marsh aliyekuwa kocha msaidizi wa Taifa Stars, aliyefariki dunia Machi 14, mwaka huu, wameingia kwenye gogoro zito la kugombania fedha zilizotolewa na Klabu ya Simba kama ubani kwa Kituo cha Marsh Athletic Centre alichokuwa akikimiliki.


Hali hiyo imezua zogo baada ya baadhi ya ndugu wa marehemu kudai kuwa kiasi hicho cha fedha walitakiwa wakichukue wao na siyo kwenda kwenye kituo.

Simba ilitoa ubani huo baada ya kutembelea hivi karibuni kisha kuahidi kutoa seti ya jezi pamoja na mipira katika kituo hicho, lengo likiwa ni kuthamini mchango wa Marsh na kuendeleza soka mkoani Mwanza.

Kaka wa Marsh aliyejitambulisha kwa jina la Melcior Dionizi Marshishigulu alisema kiasi hicho cha fedha kilistahili kwenda kwenye familia na siyo kwenye kituo kwa kuwa marehemu ni ndugu yao na kudai kuna watu wanatumia kituo hicho kujipatia kipato.

Msimamizi wa Marsh Academy, Ahmad Ally ‘Ostaadhi’ alipoulizwa alisema: “Simba waliahidi kutoa ila hawajatoa hizo fedha wala hawajatupa hiyo mipira, hapa nilipo nipo nashona mpira ili twende mazoezini, kuhusu masuala ya ndugu siwezi kusema lolote, hayo ni mambo ya familia yao na hayanihusu.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic