April 9, 2015


Kocha wa zamani wa Simba, Zdravko Logarusic amesema yeye ataendelea kuwa shabiki wa Simba milele.


Akizungumza na SALEHJEMBE kutoka Nairobi, Kenya Loga amesema mapenzi yake katika soka la Tanzania yanabaki kwa Simba.

"Naipenda sana Simba, nilijua ningefanya mambo mengi makubwa ila ndoto zangu zilikatizwa na viongozi ambao nasema hawakujua wanachofanya.

"Najua hadi leo watakuwa wanakumbuka mambo kadhaa na ikiwezekana ndiyo wanayoyatumia. Sikuona walichofanya kunitoa mimi na kumleta yule Mzambia (Patrick Phiri). Sijui tofauti ilikuwa ni ipi.

"Lakini siwezi kulazimisha kazi, nilikasirika sana, hadi leo naamini haikuwa sahihi. Bado hiyo haiondoi mapenzi yangu kwa Simba kwa kuwa mashabiki na wanachama pia waliniunga sana mkono," alisema.

Kwa sasa Loga anainoa AFC Leopards ya Kenya ambayo imeishacheza mechi tano chini yake. Imeshinda miwili, sare mbili na kupoteza mmoja.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic