April 2, 2015


Basi lililobeba mashabiki wa Yanga wanaokwenda kuishangilia timu yao keshokutwa, tayari limewasili nchini Zimbabwe.


Basi hilo aina ya Toyota Costa ‘Mayai’ limetua kwenye mpaka wa Zimbabwe leo asubuhi na walitarajia kukanyaga ardhi ya nchi hiyo leo.

Hata hivyo, bado watakuwa na safari ndefu na wanatarajiwa kuwasili Harare leo mchana kabla ya kuanza safari nyingine ya kwenda Bulawayo ambako Yanga itapambana na FC Platinum katika mchezo wa pili wa Kombe la Shirikisho.

Mmoja wa mashabiki walio katika basi hilo amesema wamekuwa wakiendelea vizuri. Msafara wa basi hilo, pia yumo mzee wa Yanga, Ibrahim Akilimali ambaye ameungana na vijana kwenda kuwapa nguvu Yanga.


Yanga itashuka dimbani Jumamosi kuhakikisha inalinda ushindi wake wa mabao 5-1 ilioupata jijini Dar ili isonge mbele.

1 COMMENTS:

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic