Timu mbili za Etoile du Sahel na ndugu zao Esperance zitapata nafasi ya kuizungumzia Yanga zikiwa katika ndege moja, kesho.
ETOILE |
Etoile du Sahel ambayo itacheza na Yanga katika mechi ya Kombe la Shirikisho kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar, Jumamosi, itapanda ndege moja na Esperance ambayo inakwenda Sudan kuivaa El Merreikh.
Ndege hiyo itaanzia jijini Kharthoum kuwashusha Esperance, halafu itachanga anga hadi jijini Dar es Salaam na kuwasubiri Etoile kabla ya kuwapitia tena Esperance na kurejea kwao Tunisia.
ESPERANCE |
Esperance iliifunga Yanga mabao 3-0 katika Ligi ya Mabingwa Afrika mwaka 2009 na kuing'oa katika michuano hiyo.
Hivyo itakuwa lahisi Waarabu hao kukumbushana kuhusiana na Yanga wakati wakiwa njiani kwenda Sudan na baadaye kuja nchini.
Timu hizo zinakaa katika miji tofauti, wakati Esperance inatokea mji mkubwa zaidi nchini Tunisia wa Tunis, Etoile wanatokea katika mji mdogo wa Sousse.
0 COMMENTS:
Post a Comment