Jurgen Klopp amekubali kuachia ngazi kuinoa timu yake kipenzi ya Borussia
Dortmund.
Klopp mwenye umri wa miaka 47, amekubali kuondoka katika kikosi
hicho wakati wa majira ya joto.
Raia huyo wa Ujerumani amesema ataondoka ramsi Juni 30 na kuiacha
BVB aliyoifundisha kwa miaka saba.
Hali imekuwa ikienda mwendo wa kusua katika kikosi hicho na Klopp
amekubali na kusema Dortmund: “inahitaji mabadiiko.”
Haikuwa lahisi kwa kocha huko kukaa na kuzungumza na wachezaji
wake kuwaeleza kwamba ataondoka mwishoni mwa msimu.
Akiwa na Dortmund ameiwezesha kubeba ubingwa wa Ujerumani mara mbili
pamoja na Kombe la Ujerumani.
0 COMMENTS:
Post a Comment