SHIBOLI WAKATI AKIITUMIA AFRICAN SPORTS MSIMU ULIOPITA. |
Straika wa zamani wa Simba, Ahmed Shiboli amesaini
mkataba wa miaka miwili kuichezea Coastal Union.
Shiboli amesema amejiunga na Coastal ambayo msimu uliopita ilikuwa ikipambana kuhakikisha inabaki Ligi Kuu.
Pia Msemaji wa Coastal Union, Oscar Asenga amesisitiza kwamba wanaamini Shiboli atawasaidia.
"Ni mmoja wa washambuliaji wakongwe hapa nchini. Tuna imani atatoa msaada," alisema.
Kabla ya kutua Coastal Union, Shiboli alikuwa tegemeo la wapinzani wao wakubwa African Sports ambao wamerejea Ligi Kuu Bara.
0 COMMENTS:
Post a Comment