May 30, 2015


Klabu ya African Sports ya Tanga, ikiwasisitiza wachezaji mbalimbali kujitokeza kusajiliwa na timu hiyo iliyopanda kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao.


Meneja wa timu hiyo, Ahmed Bosnia, amesema kuwa, wachezaji hao wanatakiwa kufika mazoezini na atakayeonekana mzuri atasajiliwa kwa dau nono.

"Hatuwezi kujua nani ana uwezo zaidi, ila tunatoa nafasi waungane nasi mazoezini na mwisho watapatikana wanaohitajika.

"Tayari benchi la ufundi litakuwa linashughulika na nini kinachotakiwa lakini bado tunatoa nafasi kwa wengine zaidi," alisema Bosnia.

Sports imerejea Ligi Kuu Bara baada ya kushika nafasi ya pili katika Ligi Daraja la Kwanza nyuma ya mabingwa Mwadui FC ya Shinyanga.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic