Mtanzania Francis Cheka amefanikiwa
kumtwanga Mthailand, Kiatchai Singwancha kutoka Thailand katika pambano lililo
la ubingwa.
Cheka ameshinda kwa Technical
Knockout (KO) baada ya Singwacha kushindwa kuendelea na pambano katika raundi
ya nane.
Mara baada ya kwisha kwa raundi ya
saba, Singwacha alitangaza kushindwa kuendelea na raundi ya nane, hivyo kufanya
Cheka kupata ushindi huo wa KO.,
Tokea mwanzo, Cheka kutoka Morogoro,
alionekana kuwa makini zaidi huku akipiga ngumi za kuvizia.
Cheka ambaye ametoka jela na hili ni
pambano lake la kwanza alizidi kumpa wakati mgumu Mthai huyo kila raundi
zilivyokuwa zikiongezeka hadi aliposalimu amri.
0 COMMENTS:
Post a Comment