Kiungo mkabaji wa zamani wa Simba na Yanga,
Athumani Idd ‘Chuji’, amepanga kufunga safari kwenda mkoani Shinyanga kwa ajili
ya kusaini mkataba mpya wa kuichezea timu hiyo msimu ujao kwenye Ligi Kuu Bara.
Mchezaji huyo ni miongoni mwa wachezaji
wakongwe walioiwezesha timu hiyo kupanda kucheza Ligi Kuu Bara msimu ujao,
wengine ni Monja Liseki, Juma Jabu, Abdallah Kigodeko na Uhuru Selemani.
Chuji amesema:
“Juni 9 nitaenda kusaini mkataba Mwadui kwani uongozi umeniambia nifanye hivyo
mimi na wenzangu wote ambao tupo Dar es Salaam.
Hata hivyo Chuji alisisitiza kabla ya kusaini, watajadiliana suala la maslahi kama ilivyo kawaida, kama watakubaliana abasi atafanya hivyo.
“Hatutasaini kichwakichwa kwani
tutazungumza kwanza kuhusu maslahi.”
0 COMMENTS:
Post a Comment