May 30, 2015


Uongozi wa Coastal Union umetangaza kuwatema kipa wake namba moja Shabani Kado na washambuliaji wake raia wa Kenya na Mkongo.


Mganda Yayo Kato na Mkongo, Itubu Imbem, Seleimani Kibuta, Razack Khalfani, Keneth Masumbuko na Othumani Tamimu.

KIKOSI CHA COASTAL MIAKA MIWILI ILIYOPITWA. ASILIMIA 70 YA WACHEZAJI HAWA HAWAPO. SASA WALIOONGEZWA, NAO WAMETEMWA KWA ASILIMIA 40.
Wengine walioachwa ni Hussein Sued, Mansour Alawi, Amani Juma, Mohamedi Mtindi na Mohamed
Hassani.


Kikao cha Kamati ya Utendaji cha Coastal Union ambacho kimeketi katikati ya wiki hii chini ya Makamu Mwenyekiti wa Coastal Union, Steven Mguto kimeazimia kuwaacha baadhi ya wachezaji ambao muda wao ulikuwa umemalizika huku wengine wakiongezewa mikataba ya kuendelea
kuitumikia timu hiyo kwa msimu ujao.

Kimsingi wachezaji hao wameachwa na sasa wapo huru kutumikia timu nyingine ambazo zitahitaji huduma zao

Akizungumza na waandishi wa habari leo, Ofisa Habari wa Coastal Union,Oscar Assenga amesema
kuwa maamuzi hayo yalifikiwa katika kikao cha Kamati ya Utendaji ya klabu hiyo ambacho kilifanyika juzi mkoani hapa.

Hata hivyo amesema wachezaji ambao wamemaliza mikataba yao ambao klabu ipo kwenye mazungumzo nao kwa ajili ya msimu ujao ni Bakari Mtama, Rama
Salim, Godfrey Wambura na Joseph Mahundi.

Wakati huo huo, uongozi wa Coastal Union umewapandisha timu wachezaji wanne kutoka timu ya vijana kucheza timu ya wakubwa ambao ni Mtenje
Albano, Tumaini Karim, Mohamed Twaha Shekue “Djong”, Fikirini Suleiman“Mapara”


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic