Waziri Mkuu Mstaafu, Edward Ngoyai Lowassa amesema atahakikisha Tanzania inaondoka katika kuitwa kichwa cha mwendawazimu.
Lowassa ameyasema hayo wakati akihutubia kwenye Uwanja wa Sheikh Amri Abeid jijini Arusha, Lowassa alisema iwapo atapitishwa kugombea kupitia CCM, basi atahakikisha anapambana na udhaifu wa Tanzania katika michezo mbalimbali hadi kufikia kuitwa kichwa cha cha Mwendawazimu.
"Kama nitapata nafasi, basi nitahakikisha Tanzania inaondokana na kuitwa kichwa cha Mwendawazimu," alisema wakati akiwahutubia wakazi wa jiji la Arusha na kutangaza rasmi nia ya kugombea Urais.
"Tanzania tumekuwa hatufanyi vizuri katika michezo mbalimbali ikiwemo riadha na michezo mingine."
Lowassa ni kati ya wanachama wa CCM wanaowania nafasi hiyo ya urais kupitia CCM.
Wakazi wa jiji la Arusha walijitokeza kwa wingi sana kwenye uwanja huo kumsikiliza akitangaza nia yake hiyo ya kuwania urais.
0 COMMENTS:
Post a Comment