Shirikisho la Soka Afrika (CAF), leo hii limeipa Tanzania uenyeji wa fainali za michuano ya Afrika
ya vijana umri chini ya miaka 17 mwaka 2019.
Uenyeji huu ni hatua muhimu sana kwa
Tanzania katika kukuza soka la vijana na kwa hatua hii Tanzania itacheza moja
kwa moja fainali hizi.
Katika kuandaa kikosi bora cha kushiriki
fainali hizi Tanzania, mwezi Juni mwaka huu TFF itaandaa mashindano ya Taifa ya
vijana umri chini ya miaka 13 na wachezaji bora wa mashindano haya wataunda
kikosi cha mwanzo cha Taifa kuelekea fainali za mwaka 2019.
TFF inamshukuru sana Rais Jakaya Kikwete
na Mh. Fennela Mukangara Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa
kufanikisha maamuzi haya, na inaamini ushirikiano huu wa Serikali na wadau
wengine utafanikisha mashindano haya mwaka 2019.
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA
MIGUU TANZANIA (TFF)
0 COMMENTS:
Post a Comment