Kiungo mpya wa Yanga, Deus Kaseke ameongezwa katika
kikosi cha timu ya taifa kinachojiandaa kuivaa Misri.
Pamoja na Kaseke ambaye amejiunga Yanga kwa dau la Sh
milioni 35 akitokea Yanga, wengine watatu wameongezwa na wote wameanza mazoezi leo kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam.
Wengine walioongezwa katika kikosi hicho ni kipa wa
Mtibwa Sugar, Said Mohammed pia beki wa timu hiyo Andrew Vincent na kiungo wa
Azam FC, Gardiel Michael.
Kocha Mkuu wa Taifa Stars, Mart Nooij ambaye amekalia
kuti kavu kutokana na kikosi chake kwenda mwendo wa kusua, ameamua kuimarisha
kikosi chake na imeelezwa atafanya mchujo kabla ya kwenda Misri.
0 COMMENTS:
Post a Comment