Simba
imemsajili kipa namba moja wa Mohammed Abrahman Mohammed wa JKU.
Kipa
huyo amesaini mkataba wa miaka miwili leo mbele ya Mwenyekiti wa Kamati ya
Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ofisini kwake Mbezi Beach jijini Dar es Salaam.
Hans
Poppe amesema wamemsajili kipa huyo kuimarisha safu yao ya ulinzi.
Ingawa
hakuzungumzia lolote kuhusiana na wingi wa makipa, kutua kwa Mohammed, maana
yake ni safari kwa kipa Hussein Shariff ‘Casillas’ ndiyo anaondoka Simba.
Mzanzibari
huyo anafanya idadi ya makipa wa timu kubwa ya Simba kufikia wanne.
Pamoja
na yeye ni Ivo Mapunda, Peter Manyika na Casillas ambaye inaonekana safari
imemkuta.
,
0 COMMENTS:
Post a Comment