Ile kesi iliyopo kwenye Mahakama ya Kazi jijini Dar ambayo Klabu
ya Yanga imewashtaki wachezaji wake Juma Kaseja na Mbrazili, Geilson Santana
‘Jaja’, inatarajiwa kusikilizwa leo Jumatano kwenye mahakama hiyo.
Awali, kesi ya Jaja ilikuwa inaahirishwa mara kwa mara baada ya
mtuhumiwa kuwa mbali huku akiomba kupewa muda wa kutuma mwakilishi au kuja
mwenyewe ambapo kesho ni hatua ya mwisho na kama mtu kutoka upande wake
akishindwa kutokea mahakamani, basi kesi hiyo itasikilizwa kwa upande mmoja.
Jaja anatuhumiwa na Yanga kwa kuvunja mkataba kinyemela ambapo
anatakiwa kuwalipa Yanga milioni 57, hali kadhalika kwa Kaseja ambaye alikiuka
masharti ya mkataba, anatakiwa kuilipa Yanga milioni 300.
Mwanasheria wa Yanga, Frank Chacha, ameliambia Championi Jumatano
kuwa, kuelekea kwenye kesi hiyo, kila kitu kwa upande wao kinaenda sawa na
kinachosubiriwa ni wakati ufike ili haki itendeke.
“Kesi ya Jaja baada ya hatua ya usuluhishi kupita, sasa ipo hatua
ya maamuzi ambapo kama akishindwa kufika basi tutaiomba mahakama kesi
isikilizwe upande mmoja,” alisema Chacha.
Kuhusu kesi ya Kaseja, Chacha alisema ipo kwenye hatua ya maamuzi
ambapo hatua ya kwanza kila mtu amewasilisha maelezo ya awali ambapo leo wanakutana
kwa ajili ya kupambanisha hoja za mdai na mdaiwa mpaka itakapofikia hatua ya
kuletwa mashahidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment