Uongozi wa Simba umepokea maombi ya makocha
kutoka mataifa mbalimbali kwa ajili ya kumrithi Mserbia, Goran Kopunovic, kati
ya hayo yumo Mmarekani mmoja.
Timu hiyo, hivi sasa ipo kwenye mchakato wa
mwisho wa kukamilisha mchujo wa kumpata mbadala wa Kopunovic atakayekinoa
kikosi hicho baada ya kuachana na Mserbia huyo ambaye walishindana naye dau
kufuatia kumalizika kwa mkataba wa muda mfupi aliosaini awali.
Makamu wa Rais
wa Simba, Geofrey Nyange ‘Kaburu’, alisema Mmarekani huyo yupo kwenye orodha ya
majina ya makocha wanaotaka kurithi kibarua cha Kopunovic.
Kaburu alisema kuwa, pia wamepokea maombi ya
kocha kutoka nchini Asia ambaye anatimiza idadi ya makocha 100 wanaotaka
kuifundisha timu hiyo.
“Ipo kamati husika inayohusika na mchakato huo wa
kumpata kocha mpya atakayeifundisha Simba, hadi hivi sasa imefikia idadi ya
makocha 100.
“Makocha wa mataifa mbalimbali wamejitokeza
kiukweli, yupo kutoka Marekani na Asia ambao wote tunaamini ni wazuri, yupi
atakayekabidhiwa? Tuiachie kamati inayohusika na mchakato huo,” alisema Kaburu.
SOURCE: CHAMPIONI
0 COMMENTS:
Post a Comment