Siku chache baada ya kusaini kuichezea Yanga,
kiungo mshambuliaji, Deus Kaseke, ametamka kuwa anaitumia timu hiyo kama njia
kwake ya kwenda kucheza soka la kulipwa Ulaya kwa kuwa Yanga itashiriki
michuano ya kimataifa.
Kaseke amesaini Yanga kwa mkataba huo wa miaka
miwili kwa dau la shilingi milioni 35 licha ya kuwindwa na Simba pia, amedai
kuwa ndoto zake zilikuwa ni kuichezea moja ya klabu kubwa nchini ili aonekane
na apate soko la kucheza nje ya nchi.
“Ilikuwa ni ngumu kwenda kusaini kuichezea Simba
kwa ajili ya msimu ujao na sijutii maamuzi niliyoyachukua ya kusaini Yanga
kutokana na malengo yangu niliyojiwekea katika soka.
“Ndoto zangu ilikuwa kuichezea timu
itakayoshiriki michuano ya kimataifa, hivyo ninaamini uwepo wangu Yanga
utafungua milango kwangu kuonekana kimataifa,” alisema Kaseke.
Yanga itashiriki katika michuano ya Ligi ya
Mabingwa Afrika kwa kuwa imetwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara wakati Simba ilishika
nafasi ya tatu, haitashiriki kimataifa katika michuano inayoandaliwa na
Shirikisho la Soka Afrika (Caf) ikiwa ni mwaka wa tatu mfululizo.
0 COMMENTS:
Post a Comment