Kampuni ya Azam Media, jana ilitangaza rasmi
kuanza kwa michakato ya msimu wa pili wa Kwetu House utakaokuwa na vitu vingi
vipya vitakavyoongeza utamu wa shindano hilo linalotarajiwa kuruka hewani
kwenye stesheni za Azam.
Uzinduzi huo wa shindano hilo ambalo safari hii
litajumuisha jumla ya mikoa mitano zaidi kwa ajili ya kunogesha na kuleta
upinzani wa kutosha, ulifanyika kwenye Ofisi za Azam zilizopo Tazara jijini
Dar.
Mkurugenzi wa Azam, Rhys Torrington, alifafanua
baadhi ya mambo, ikiwemo jinsi ya kuwapata washiriki wa shindano hilo ambalo
hujumuisha zaidi wapenzi wa soka na kuweka wazi kuwa msimu huu mshindi
ataondoka na kitita cha shilingi milioni 15, tofauti na msimu uliopita ambao
ilikuwa Sh milioni 10.
“Msimu huu kutakuwa na vitu vingi zaidi kwa ajili
ya kuboresha na kuyanogesha haya mashindano, kutakuwa na jumla ya washiriki 20
wakijumuishwa wanawake pia. Vilevile msimu huu wataongezeka washiriki kutoka
mikoa ya Mbeya, Dodoma, Arusha, Mwanza, Dar na hata Zanzibar.
“Mchujo wa kutafuta washiriki utafanyika katika
kipindi chote cha Juni na kisha shindano lenyewe litachukua siku 45, kwa ajili
ya kujua zaidi kuhusiana na mchujo tunaomba Watanzania waendelee kuangalia
stesheni za Azam kwa ajili ya kupata taarifa zaidi,” alisema Torrington.
0 COMMENTS:
Post a Comment