Kamati ya Nidhamu ya
Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini TFF iliyoketi jumanne tarehe 5 Mei, 2015
imempiga faini ya sh. 5,000,00 (milioni tano), Afisa Habari wa klabu ya Yanga
SC Jerry Muro kwa kutoa kauli za chuki, kisirani na uchochezi dhidi ya uongozi
wa Bodi ya Ligi (TPLB) nchini na TFF.
Akitoa utetezi wake
mbele ya Kamati ya Nidhamu, Jerry Muro alikiri na kujutia kufanya kosa hilo na
kudai ilitokana na ugeni wake katika uongozi wa michezo, kwa kuzingatia hilo
kamati ilimuepusha na adhabu ya kufungiwa..
Kwa mujibu wa Ibara ya
53 (2)ya Kanuni za Nidhamu za TFF toleo la 2012, kwa kuidhalilisha TFF na Bodi
yake ya Ligi mbele ya umma, kamati imemtoza faini ya sh. 5,000,000 (millioni
tano), Jerry Muro na kuwaonya viongozi wengine wa familia ya mpira wa miguu
kutojihusisha na vitendo vya matamshi ya aina hiyo.
Shitaka linalomhusisha
mchezaji wa Yanga, Amissi Tambwe kumshika kwa kumdhalilisha mchezaji wa Simba
SC Juuko Mursheed, na kiongozi wa Friend Rangers Hery Chibakasa wa Friends
Rangers kuhamasisha vurugu katika mchezo wa timu yake na dhidi ya Majimaji ya
Songea Januari 29, 2015, kamati imeahirisha mashitaka hayo mpaka tarehe
nyingine itakapopangwa.
Kamati iliahirisha
malalamiko dhidi ya Mohamed Hussein, Muhibu Kanu, Manfred Luambano, Venance
Joseph, Mussa Senyange, Saleh Ali, Shafii Maganga na Ismail Salim baada ya
kupokea taarifa za udhuru zilizosbabishwa na mgomo wa madereva wa mabasi ya
abiria ya mikoani.







0 COMMENTS:
Post a Comment