Maofisa
sita wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) wamekamatwa jijini Zurich kwa
tuhuma za rushwa.
Maofisa
hao akiwemo Makamu wa Rais wa Fifa, Jeffrey Webb wametiwa nguvuni na Jeshi la
Polisi la Uswis, leo saa 12 alfajiri.
Maofisa
hao walikamatwa katika hoteli moja ya kifahari na kutolewa huku wakiwa
wamefunikwa kwa shuka na wafanyakazi wa hoteli hiyo ili wasipigwe picha.
Inaelezwa
wanatuhumiwa kupokea rushwa ili kutoa nafasi kwa mashindano ya Kombe la Dunia
mwaka 2018 nchini Urusi na 2022 yatakayofanyika nchini Qatar kufanyika katika
nchi hizo.
Pia
imeelezwa memba wengine 10 wa kamati ya utendaji ya Fifa watahojiwa.
![]() |
| MAKAMU WA RAIS WA FIFA AMBAYE NI RAIS WA CONCACAF, NAYE AMTIWA MBARONI. |
Madai
hayo yameongeza kwamba maofisa hao wanaaminika kuchota rushwa hadi ya dola
milioni 100 kwa ajili ya kuizipa nchi hizo nafasi.
Msemaji
wa Fifa, Walter de Gregorio amesema licha ya maofisa hao kutiwa mbaroni,
komgamano la kesho Ijumaa kuhusiana na uchaguzi wa Rais wa Fifa litaendelea
kama kawaida.
Rais
wa sasa wa Fifa, Sepp Blatter ndiye anayepewa nafasi kubwa kushinda kwa muhula
wa tano mfululizo.











0 COMMENTS:
Post a Comment