Wakati harakati za usajili zinazidi kupamba moto, mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga
wanaonekana kuwa ndiyo waliomwaga fedha nyingi zaidi katika kipindi cha
usajili.
Yanga
wamemwaga zaidi ya Sh milioni 195 katika fedha zao ambazo wametumia kwa ajili
ya kuimarisha kikosi chao na watamwaga zaidi ya hizo hadi watakapokuwa
wamemaliza.
Gharama
zinaweza kufikia zaidi ya Sh milioni 200 hadi sasa kama itajumlishwa na fedha
walizowatumia wachezaji kwa ajili ya usafiri kutoka katika miji ya Mbeya,
Zanzibar na pia kuwasafirisha wengine.
Wako ambao
waliboresha mikataba yao na wengine wapya ambao tayari wameishatua Jangwani kwa
ajili ya msimu ujao.
Kwa upande wa
Simba, nao wanaonekana kujitutumua kwani katika fedha kwa ajili ya kuimarisha
kikosi chao ukianzia zile za Jonas Mkude hadi sasa, tayari wametoa zaidi ya Sh
milioni 165.
Simba
wameboresha baadhi ya mikataba ya wachezaji wao lakini inaonekana pia bado
wanaweza kufikia Sh milioni 200 na zaidi kwa kuwa bado wanahitaji kuboresha
mkataba wa Ramadhani Singano ‘Messi’, Ivo Mapunda na pia kusajili wachezaji
wapya.
Yanga (Sh
milioni 195):
Deus Kaseke
kutoka Mbeya City (Sh milioni 35), Haruna Niyonzima (Sh milioni 70), Mbuyu
Twite (Sh milioni 30), Deogratius Munish ‘Dida’ (Sh milioni 20) na Benedict
Tinocco kutoka Kagera (Sh milioni 20) na Haji Mwinyi Mgwali kutoka KMKM (Sh
milioni 20).
Simba (Sh
milioni 165):
Jonas Mkude
(Sh milioni 60), Said Ndemla (Sh milioni 30), Hassan Isihaka (Sh milioni 30),
Paul Mwalyanzi kutoka Mbeya City (Sh milioni 25), William Lucian ‘Gallas (Sh
milioni 20).
0 COMMENTS:
Post a Comment