May 27, 2015

WAKATI WA UHAI WAKE, SHEIKH OMARY.

Mwenyekiti mpya wa Villa Squad, Sheikh Omar Alhady amefariki dunia katika Hospital ya Taifa ya Muhimbili.
Taarifa zilizotolewa na uongozi wa klabu hiyo yenye makao yake makuu Magomeni jijini Dar es Salaam zimeeleza marehemu alikwua akisumbuliwa na tatizo la figo.


SHEIKH OMARY (WA TATU KULIA) AKIWA NA VIONGOZI WENGINE WA VILLA, GODIGODI (KULIA), IDD MOSHI ANAYEMFUATIA NA VIONGOZI WENGINE.

Sheikh Omary alichaguliwa kuwa mwenyekiti katika mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika Mei 17, maana yake amekaa madarakani kwa siku kumi tu.

Enzi za uhai wake Sheikh Omary alikuwa ni mmoja wa masheikh mashuhuri nchini pia alikua ni Imàm katika msikiti wa Kichangani jijini Dar es Salaam.
 
...AKIWA NA VIONGOZI WENGINE WA DINI, RAIS MSTAAFU ALI HASSAN MWINYI NA MAKAMU WA RAIS, GHALIB BILAL.Villa wameeleza kupokea taarifa hizo kwa masikitiko makubwa huku wakisema hawana namna zaidi ya Kumuombea dua ili Mwenyezi Mungu amuepushe na adhabu za kaburi na ahela.

IMETOLEWA NA BOSI WA MAWASILIANO WA VILLA SQUAD, IDDI GODIGODI.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic