Simba imetangaza kumsajili kwa mara nyingine
mshambuliaji wake wa zamani, Mussa Hassan Mgosi.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya
Simba, Zachakaria Hans Poppe amekubali kwamba Mgosi wamekubaliana kwa mwaka
mmoja.
“Tumeshamalizana na Mgosi, tumemrudisha kundini. Kweli
tumeridhishwa na kazi yake kwa msimu uliopita.
“Lengo ni kuwa na wakongwe ambao watasaidiana na
vijana, tunataka kufanya naye kazi kwa mwaka mmoja,” alisema.
Hata hivyo, Mgosi alisema kwamba hadi Jumatatu, ndiyo
atakuwa amemaliza na Simba.
“Kweli ni hivyo lakini hadi Jumatatu tunaweza tukawa
tumemmalizana na Simba, nitakueleza vizuri ikiwa tayari,” alisema Mgosi.
0 COMMENTS:
Post a Comment