Na
Saleh Ally
SIMBA
imeanza usajili kwa ajili ya kuimarisha kikosi chake, kabla ya kuanza kusajili
wachezaji wapya, imeanza na wachezaji wake kwanza.
Uongozi
wa Simba umelazimika kuanza kuwaongezea mikataba wachezaji wake kwanza ambao
imekuwa nao kabla ya kuanza kusajili wapya.
Hali
inavyokwenda imeonekana wachezaji ambao wamekulia Simba ndiyo wamekuwa ghali
zaidi hata kuliko wale wageni!
Kitendo
cha wachezaji wa zamani waliochezea Simba kuwa ghali zaidi kimenifanya
nitafakari mambo mengi sana, lakini matatu huenda yakawa ya msingi sana.
Muda:
Vijana
waliotakiwa kuongezewa mikataba Simba, wengi walibadilika na kutaka fedha
nyingi sana ambazo huenda Simba ingetoa chini ya hapo na kupata wachezaji
wengine.
Vizuri
kwa kuwa wakati unawaruhusu na vijana nao wanataka maendeleo hivyo ni lazima
wapambane kuhakikisha wanapata nafasi ya maisha mazuri.
Ndiyo
maana ulisikia Jonas Mkude akifikia hadi Sh milioni 60, Said Ndemla na Hassan
Isihaka, kila mmoja Sh milioni 30 na wengine pia walionekana kutaka fedha
nyingi zaidi.
NDEMLAKwangu naona sawa kwa vijana kupata maslahi mazuri, lakini bado nabaki kutaka kujua kila aliyepata anastahili? |
Msaada:
Timu
nyingi za Ulaya si rahisi kusikia zimetoa fedha nyingi au kubwa sana kumsajili
mchezaji ziliyenaye, badala yake huongezewa maslahi makubwa hasa katika
mshahara na kipato kama posho na mengineyo.
Kwa
Simba, wachezaji wengi walitaka fedha kubwa za usajili ambazo hata kama Simba
ingetaka mchezaji kutoka nje, basi ingempata kwa fedha hiyo au chini yake.
Mfano,
Simba imefanya usajili wa mchezaji kutoka Mbeya City, imemlipa chini ya fedha
ilizowalipa wachezaji iliyonao na hii inaonekana ni presha kutoka nje. Kwamba
Simba wakimuacha fulani, Azam FC au Yanga watamchukua na wenyewe wataonekana
hawana lolote kwa wanachama wao!
Lakini
jiulize, Simba iliyoacha kusajili wachezaji wazoefu igombee ubingwa, ikaamua
kubaki na wachezaji makinda kwa misimu mitatu mfululizo, Simba haijawa na
mafanikio yoyote!
ISIHAKA. |
Imekosa
mafanikio kwa kuwa ilisema inawakuza wachezaji. Sasa ilikuwa inawakuza ili
iweje kwa kuwa kama ni kutoa fedha, mwisho imesajili kwa gharama sawa au zaidi
na ingetaka wachezaji wapya kutoka nje ya timu. Kwa kipengele hiki naona Simba
imepata hasara.
Naweza
kushauri kwamba kunalazimika kuwa na hesabu za kitaalamu zaidi kuliko kuangalia
wanachama watasemaje. Simba lazima iwe inajali suala la faida hata kama ni
vizuri vijana kupata maslahi mazuri.
Kama
imemsajili Mkude kwa Sh milioni 60, Simba ina uhakika wa kumuuza Sh milioni
150? Kwa kuwa kama haina uhakika, itakuwa imepata hasara mara mbili. Imemkuza
halafu ikamnunua yenyewe na mwisho ishindwe kumuuza!
Hasara:
Yanga
imepata hasara kwa Mrisho Ngassa ingawa wengi wamelichukulia hilo kama jambo la
kawaida tu. Kamwe hauwezi kumuacha mchezaji kama huyo aende akiwa free, wewe
usipate hata senti, si sahihi.
Simba
inaweza kuingia katika kundi hilo la kupata hasara mfululizo kwa kuwa pia
iliwahi kumuongezea Emmanuel Okwi mkataba kwa dola 40,000 (Sh milioni 81),
ikatangaza kumuuza ‘bure’ kwa dola 300,000 (Sh milioni 608) kwa Etoile du Sahel
lakini hadi leo haijapata kitu!
Si
ajabu siku fulani ukasikia Mkude au Ndemla akiondoka Simba kama mchezaji huru,
itakuwa kichekesho.
Kukuza,
faida yake kubwa ni kuuza. Mfano mzuri ni Barcelona na Cesc Fabregas, ilimuuza
akiwa kinda, akakuzwa Arsenal nao wakamuuza tena Barcelona, ikamtumia halafu
ikamuuza tena Chelsea. Utaona mchezaji huyu mmoja alitengeneza mamilioni ya
fedha.
Kama
Simba haitawauza wachezaji hao, itakuwa imepata hasara kwa kuwa tayari
imewasajili kwa fedha nyingi zaidi kuliko hata kama ingewanunua kutoka nje ya
timu. Unaweza kuifananisha na hadithi ya samaki anayekaanga mafuta!
Klabu
ni taasisi inayopaswa kuingiza faida, si kujifurahisha tu. Kama wachezaji hao
wanaigharimu Simba fedha nyingi kuliko ingeleta wengine kutoka nje, hiyo ni
hasara kimahesabu kwa kuwa miaka mitatu yote imeingia hasara ya kushindwa
kucheza michezo ya kimataifa kwa kuwa ilikuwa ikiwakuza vijana ambao haistahili
kugharimika tena kwa kiasi kikubwa labda tu kama ina uhakika wa kuwauza.
Je,
hao iliowanunua kwa fedha nyingi baada ya kuwakuza kisoka, ina uhakika itawauza
na kurudisha fungu lake?
Bado
natetea maslahi ya vijana wa Kitanzania, kwamba akina Mkude, Ndemla na wenzake
kupata maslahi mazuri ni jambo jema, lakini wao pia wanapaswa kukumbuka kuwa
wana deni na klabu hiyo.
Maana
imewakuza, halafu ikawapa nafasi ya kucheza na kuonekana, ndiyo maana leo
wanajiona ni watu wakubwa.
Kupewa
tu nafasi ni jambo kubwa sana. Sasa wamenunuliwa tena utafikiria wanatokea nje
ya Simba! Swali langu wanatambua Simba imegharimika kwa ajili yao na wana deni
kubwa?
Wachezaji
wengi sana hujisahau kutokana na gharama yao baada ya kuuzwa au kununuliwa!
Hawa wa Simba wanajua deni lao, kwamba Simba haikushiriki michuano ya kimataifa
kwa kujaza vijana. Sasa wao wanalipwa kama mastaa, wataisaidia ibadilike na
kushiriki michuano ya kimataifa?
Ungetafakari ya Man Utd na Pogba pengine ungebadili mawazo yako na kukubali kuwa Simba haifanyi makosa ila inalinda ilichonacho....
ReplyDeleteTatizo ni uelewa wa viongozi wetu wa soka na mikataba wanayoingia!! Agharabu club kumnunua mchezaji wake mwenyewe!! Leo eti arsenal wamlipe walcot pesa ya usajili!!?
ReplyDeleteSaleh unaamini maneno ya Zakharia HansPope kwamba Singano hana thamani ya tsh.10,000,000/-?
ReplyDeleteNyie waandishi mnachekesha. wachezaji wetu wakinunuliwa bei ndogo mnapiga kelele, bei kubwa makelele, sasa mnataka nini? alafu Jonas Mkude amesajiliwa lini? usituchanganye. unapenda kufurahisha watu?
ReplyDeleteWote mnaoona simba wanakosea, usipowaongezea hao wachezaji mikataba kwa kuwapa hela unafikiri Azam Yanga na wengine watawaacha tu kwa sababu walikuzwa na simba? Msifananishe mazingira ya bongo na ulaya wakati setup ya mpira wetu na huko ni tofauti kabisa. Hebu toeni alternative kuwa simba wangefanyaje kuwabakiza hao wachezaji bila kuwapa hela. Ulaya wachezaji wengi hawapati signing on fee kwa sababu mishahara yao ni mikubwa sana
ReplyDelete