Stand United imetamba kuwa msimu ujao hautakuwa wa kugombea kuteremka daraja kama ilivyokuwa msimu huu.
Mkurugenzi wa Ufundi wa Stand United, Muhimu Kanu amesema wana kila sababu ya kufanya vizuri kwa kuwa wanajua wapi pa kurekebisha.
"Tunaweza kusema hatukufeli hata kidogo kwa kuwa lengo letu lilikuwa ni kuwania kubaki katika ligi kuu, hilo limefanyika.
"Msimu ujao hauwezi kuwa hivyo, tunajua wapi pa kurekebisha na kutengeneza kikosi bora ambacho sasa kitakuwa ni cha kuwania ubingwa na si vinginevyo," alisema Kanu.
Stand imefanikiwa kuondoka katika janga hilo katika hatua ya mwisho baada ya kuitwanga Ruvu Shooting kwa bao 1-0 katika mechi yake ya mwisho ya Ligi Kuu Bara kwenye Uwanja wa Kambarage.
0 COMMENTS:
Post a Comment