SEHEMU YA MITAA AMBAYO AMEJENGA BARABARA KWA FEDHA YAKE YA MFUKONI |
Na
Saleh Ally
KAWAIDA
wanasiasa ndiyo wamekuwa watu wenye ahadi nyingi sana linapofika suala la
maendeleo kwa jamii.
Mara
nyingi wamekuwa wakieleza namna wanavyoweza kuwapatia manufaa wananchi kama
watawachagua, mfano kuhakikisha wanapata maji safi, barabara bora na
vinginevyo.
Wanasiasa
wanajulikana kwa kutotekeleza ahadi zao na wengi wao wamekuwa wakishindwa
kuzitekeleza kwa kutoonekana kabisa baada ya kupewa kura.
Halafu,
wanaonekana kipindi kama hiki cha uchaguzi kwa kuwa kwa mara nyingine wanataka
kupata kura, yaani wachaguliwe tena.
Kabla
ya uchaguzi mkuu ambao unatarajia kufanyika Oktoba, mwaka huu, huenda wanasiasa
wanaweza kujifunza kupitia Yusuf Said Bakhresa.
Yusuf
ambaye ni mmoja wa wamiliki wa klabu ya Azam FC na Azam Media Group inayomiliki
Azam TV, ameamua kumwaga takribani Sh milioni 400 kwa ajili ya ujenzi wa
barabara jijini Dar es Salaam.
Yusuf
ambaye ni wakala wa kuuza wachezaji anayetambuliwa na Shirikisho la Soka la
Kimataifa (Fifa), tayari ameishajenga mitaa miwili na anatarajia kujenga
mingine miwili.
Mitaa
yote ipo katika eneo la Msasani jijini Dar es Salaam, karibu kabisa na
yalipokuwa makazi ya hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Ujenzi
wa barabara hizo umefanywa na wataalamu wa Kichina ambao badala ya kutumia lami
kama ilivyozoeleka, Wachina hao wamejenga kwa kutumia saruji, wakitupia zege
lenye unene mithili ya mikate mitatu iliyobebana!
Ujenzi
huo umeanzia kwenye mtaa unaotokea katika barabara ya Mwai Kibaki, unaingia
hadi kwenda kukutana na mtaa uliopewa jina la Ngome Road.
Mtaa
huo ndiyo kuna makazi ya milionea huyo upande mmoja akiwa amepakana na kampuni
maarufu ya upangishaji nyumba za kisasa ya Blue Mark.
Pamoja
na kutengenezwa kwa ubora wa hali ya juu, milionea huyo amehakikisha mitaa hiyo
miwili imewekewa taa na ing’ara kama New York.
Huenda
ndiyo mitaa miwili pekee inayoingia kutoka barabara kubwa yenye taa nyingi
kuliko yoyote ile jijini Dar es Salaam na Tanzania nzima.
Taa
zake pia huenda ndiyo ghali kuliko zote zilizo katika mitaa ya jiji la Dar es
Salaam kwa kuwa zinatumia mfumo wa solar, hazitegemei umeme wa Tanesco ambao
hauna uhakika, maana unaweza kukatika wakati wowote.
Kama
hiyo haitoshi, imeelezwa bajeti hiyo ya Sh milioni 400 itatumika kuitengeneza
mitaa mingine miwili ya Barakani Road na mwingine mdogo unaounganisha Barakani
Road na Ngome Road.
Ingawa
wanaoishi katika maeneo hayo wengi ni vigogo, imeelezwa Yusuf aliwachangisha
kiasi kidogo cha fedha ambacho huenda hakifiki hata asilimia 20 ya alichotoa.
“Alichofanya
ni kama kutaka kuonyesha ujirani, yaani ajue anashirikiana na watu wanaoishi
karibu yake. Lakini fedha zote anatoa yeye na hatua ya pili ni kujenga tena
mitaa hiyo miwili,” alieleza rafiki wa karibu wa Yusuf ambaye ni mmoja wa
watoto wa bilionea namba moja Tanzania na Afrika Mashariki, Said Salim
Bakhresa.
GETI LA KUINGIA NYUMBANI KWAKE |
Juhudi
za kumpata Yusuf alizungumzie suala hilo zilikwama baada ya kuelezwa yuko
safarini nje ya nchi kikazi.
Lakini
taarifa za uhakika zinaeleza, hana mpango wa kugombea udiwani wala ubunge,
badala yake alifanya hivyo kama mchango wake kwa jamii na kuboresha mazingira
ya eneo hilo analoishi pamoja na majirani zake.
JUMBA LAKE LA KISASA NA KIFAHARI ANALOISHI.... |
Ahsante mungu kwa ukarimu wako!
ReplyDelete