June 24, 2015


Kocha mpya wa Taifa Stars, Charles Boniface Mkwasa aliyechukua nafasi ya Mart Nooij ametangaza kikosi chake kipya kwa ajili ya kuivaa Uganda huku akimtema kipa Deogratius Munish ‘Dida’ na nafasi yake amemchagua Ally Mustapha ‘Barthez’.


Wengine ambao Mkwasa amewatema ni Erasto Nyoni, Amri Kiemba na Kelvin Friday kutoka Azam FC pia Oscar Joshua kutoka Yanga, Pia Ibrahim Ajibu kutoka Simba.

Waliorejea ni Kelvin Yondani pia Deus Kaseke huku akimchukua Michael Idan wa Ruvu Shooting.
Pia Samuel Kamuntu wa JKT, Juma Abdul wa Yanga na Mudathir Yahya kutoka Azam wamejumuishwa kwamba wanaweza kuitwa wakati wowote.

KIKOSI KAMILI:
Mwadini Ally-Azam
Ally Mustapha-Yanga
Mudathir Khamis-KMKM
Shomari Kapombe-Azam
Michael Haidan-Ruvu Shooting
Mohammed Hussein-Simba
Mwinyi Hajj-KMKM
Nadir Haroub-Yanga
Kelvin Yondani-Yanga
Aggrey Morris-Azam
Hassan Isihaka-Simba
Jonas Mkude-Simba
Abdi Banda-Simba
Simon Msuva-Yanga
Said Ndemla-Simba
Ramadhan Singano-Simba
Salum Telela-Yanga
Frank Domayo-Azam
Atupele Green-Kagera Sugar
Rashid Mandawa-Mwadui
Ame Ally-Azam
Deus Kaseke-Yanga


2 COMMENTS:

  1. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  2. Kama tunataka matokeo mazuri , Timu ya Taifa Stars inatakiwa kuacha mara moja kucheza mpira kama wa Barca wa pasi fupi fupi manake hatuuwezi, wachezaji wetu hawana uwezo wa kumiliki mipira , pasi mbili tatu tu wameshapoteza mipira, hawajiamini na hawatulii wakiwa na mipira, mabeki hawajipangi vizuri wanapitwa ovyo, mabeki waige namna beki ya timu ya Taifa ya Italia inavyocheza ukimpita mmoja mwingine amefika. Kwasasa timu icheze pasi ndefu , mpira utoke nyuma na upigwe mbele si katikati manake hatwezi, viungo wapeleke mipira mbele kwa kulazimisha waache mara moja tabia ya kurudisha rudisha mipira nyuma na kujidai wanajua kupasiana sehemu ya kati kati ya uwanja na nyuma, timu ilazimishe kupeleka mbele mipira kwenye goli la adui , na walazimishe kupita na washambuliaji walete purukushani golini kwa adui si kuzembea na kuogopa kuumia manake ndo kazi walioichagua. Timu iache mara moja tabia ya kurudisha rudisha mipira nyuma na kujidai wanajipanga baada ya kushindwa kupita. Tunatakiwa kulazimisha mipira iende mbele na kulazimisha purukushani za kusaka mabao, tuache kujidai tunajua kujipanga tukiwa na mipira. Tunahitaji kuwapa washambuliaji wa pembeni idadi ya krosi wanazotakiwa kulazimisha kuzipiga golini na tunatakiwa kuwapa washambuliaji wa kati idadi ya mipira wanayotakiwa kupiga golini kwa adui na mechi inapoisha tufanye tathmini mawinga wamepiga krosi ngapi na washambuliaji wamepiga mipira mingapi golini, lazima tuwe na targets na hesabu bila hivyo ni kilio tu kila siku. Wachezaji wa Timu ya Taifa wanatakiwa kujua kuwa watanzania wanachukizwa sana na matokeo mabovu ya timu yao na tunajua kuwa wachezaji wetu hawajitumi kwa kiwango kinachotakiwa , hata aje Mourinho ni kazi bure kama morali ya wachezaji iko chini hatuwezi kufunga, wachezaji wetu wanatakiwa kujiamini na kupeleka mipira mingi golini kwa adui na si kujifanya wanajua kupigiana pasi nyingi zisizo na faida. Jambo la msingi pia ni kwa TFF na wadau wa mipira kuwajali wachezaji kwa kuwapa posho zao kwa wakati na tuchague viongozi wenye dhamira ya kweli ya kuendeleza soka Tanzania manake kuna viongozi wengi wako katika medani ya soka kimaslahi tu hawana faida na soka letu. Tunahitaji mipango endelevu ya kukuza vipaji vya watoto wanaocheza soka na tuwe tukiwapandisha kutoka timu za chini kwenda timu ya taifa. Kocha aache mara moja kuchagua wachezaji kwa majina nakumilikisha namba kwa baadhi ya wachezaji wenye majina makubwa ambao kwa miaka mingi wamechezea timu ya taifa bila kuleta mafanikio yoyote, tuingize wachezaji wazuri wa timu ndogo na kuwatoa wachezaji wenye majina makubwa wa Simba na Yanga na Azam. Hapa ninaona kuna mchezaji ameitwa timu ya Taifa wakati alisababisha penati ya kizembe kwenye mechi kati ya Tanzania na Morocco na kusababisha Tanzania kufungwa na kutolewa wakati tayari tulikuwa tumewashika Morocco kwao na tulikuwa na goli moja mkononi lililofungwa na Abdi Kasim nadhani au ! Wachezaji wapewe muda wa kutazama mechi zao za nyuma na makosa yao waliyofanya waambiwe ili wasiyarudie! Mwisho ninauliza swali , hivi haiwezekani kuitoa katika mashindano timu ya Taifa Stars? ni aibu tupu kwa taifa letu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic