Hatimaye Azam FC wamefichua rasmi kuwa,
wanamvizia kiungo wa Simba, Ramadhani Singano ‘Messi’ na kwamba kama Msimbazi
wakimuacha tu, basi wao watamsajili kwa gharama yoyote kwa kuwa wanajua ana
kiwango kizuri.
Messi hivi sasa yupo kwenye mgogoro na Simba
kuhusiana na suala la mkataba. Simba inasema ina mkataba naye hadi mwakani,
wakati yeye anajua unaisha mwezi ujao huku TFF ikishindwa kutatua sintofahamu
hiyo.
Hivi karibuni Messi alionekana katika ofisi za
Azam FC akirandaranda, jambo ambalo lilitafsiriwa kuwa atakuwa amekwenda
kusaini mkataba wa kuitumikia timu hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Azam FC, Saad Kawemba
amesema kuwa Messi ni mmoja kati ya wachezaji wazuri hapa Bongo na iwapo Simba
watamuacha, wapo tayari kumsajili kwa kuwa ana uwezo.
“Messi alikuwa na matatizo na klabu yake kwa
sasa ni vyema akamalizana na uongozi wake huo ili kuweza kujua hatma yake. Ni
mmoja kati ya wachezaji wazuri.
“Iwapo ataanguka kwa kuachwa na Simba basi
tupo tayari kumsajili,” alisema Kawemba.
0 COMMENTS:
Post a Comment