Bao safi
alilofunga mshambuliaji Paul Modo Kiongera dhidi ya Muhoroni Youth,
limemhakikishia nafasi ya kurejea Simba.
Kiongera
ameifungia KCB bao safi katika mechi ya Ligi Kuu Kenya juzi ambayo ilimalizika
kwa ushindi wa mabao 3-0.
Bao hilo la
Kiongera katika mechi lilishuhudiwa na baadhi ya wajumbe wa Kamati ya Utendaji
ya Simba ambao waliamua kumfuatilia.
Kama
haitoshi, baadhi ya wajumbe hao wa kamati ya Utendaji ya Simba walikuwa
wakimfuatilia Kiongera wakiwa jijini Nairobi.
“Kweli kwa
bao lile safi, tena akiwa amecheza dakika 90, hakuna hofu tunamrudisha,”
alieleza mmoja wa wajumbe wa kamati hiyo.
Simba walikuwa wakimfuatilia Kiongera kwa ukaribu ili kupata uhakika wa uchezaji wake kabla ya kuamua wamrudishe kikosi au la.
Kiongera alipelekwa
KCB kwa mkopo mara baada ya kuumia na baadaye kwenda kutibiwa nchini India.
Awali alikuwa
akicheza dakika chache, tena akitokea benchi lakini sasa anaonekana ‘ameshakuwa
mtamu’, hivyo kuanza kucheza dakika nyingi.
0 COMMENTS:
Post a Comment