HENRY (KULIA) WAKATI AKIWA SIMBA, KABLA YA KUHAMIA MTIBWA. |
Kiungo mkongwe, Henry Joseph, ametamka wazi kwamba bado hajapata
timu tangu alipomalizana na Mtibwa Sugar msimu uliopita, lakini amekiri kwamba
atajisikia poa sana kama akienda kucheza Mwadui FC kutokana na sababu
mbalimbali.
Henry aliyewahi kutamba na Simba SC miaka ya nyuma kabla ya
kutimkia Kongsvinger ya Norway, amemalizana na Mtibwa katika msimu uliomalizika
hivi karibuni na yupo huru kutua popote lakini ameanza kwa kuitaja Mwadui
iliyopanda kushiriki Ligi Kuu Bara msimu ujao.
Henry alisema kwamba kikubwa anachovutiwa nacho Mwadui ni kwenda
kucheza na wachezaji wazoefu na wakongwe ambao wapo kwenye kikosi hicho.
“Bado sijajua kama nitaendelea na Mtibwa ama vipi, kwa sababu bado
nawasikilizia lakini hata timu nyingine pia nipo tayari kuzichezea, timu kama
Mwadui ipo poa, katika hizi zilizopanda inaonekana kama iko poa kwenye uongozi
na sehemu nyingine, ndiyo maana wamefika hapa.
“Halafu kitu kingine ina wachezaji wazoefu wa ligi ambao wengi
nafahamiana nao, kwa hiyo nikicheza sehemu kama hiyo haitakuwa taabu sana
kucheza mpira mzuri kwa kuwa wengi mno mnajuana na mnakuwa na morali ya aina
moja katika mapambano,” alisema Henry.
Mwadui iliyo chini ya kocha Jamhuri Kihwelo ‘Julio’, imepanda
kushiriki ligi kuu ikiwa na nyota wengi waliowahi kutamba huko nyuma lakini
imeongeza pia wengine.
Baadhi ya wachezaji wao wazoefu ni Shaban Kado, Athuman Idd
‘Chuji’, Uhuru Selemani, David Luhende, Nizar na Razak Khalfan, Jabir Aziz na
Rashid Mandawa.
0 COMMENTS:
Post a Comment