Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, (Taifa Stars)
kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro kimeendelea kujifua katika uwanja wa
Benki ya Biashara ya Ethiopia eneo la CMC asubuhi na jioni katika uwanja wa
Taifa wa Addis Ababa.
Stars ambayo imeweka kambi jijini Addis Ababa imekua
ikijifua mara mbili kwa siku, kuhakikisha wachezaji wanakua vizuri kuelekea
katika mchezo dhidi ya timu ya Taifa Misri mwishoni mwa wiki hii jijini
Alexandria.
Hali ya kambi kiujumla ni nzuri, wachezaji wote ni
wazima, wakiwa wenye ari, na morali ya hali ya juu katika maandalizi ya mchezo
huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON mwaka 2017.
Kocha mkuu wa Taifa Stars mholanzi, Mart Nooij amekuwa
akiwafundisha vijana wake mbinu mbali mbali kuelekea kwenye mechi dhidi ya
Misri, kuanzia sehemu ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji kuhakikisha
wanakua fit katika mchezo unaowakabili.
Ikiwa ni siku ya nne tangu Taifa Stars kuanza mazoezi
yake jijini Addis Ababa, kocha Nooij amesema anashukuru vijana wake wanamuelewa
vizuri anachowaelekeza, sasa timu inacheza mpira wa kasi na pasi za haraka
haraka, vijana wamechangamka na morali ni ya hali ya juu kambini kuelekea
kwenye mchezo unaowakabili.
Hali ya nidhamu kambini ni ya hali ya juu, wachezaji
waanatambua umuhimu wa mchezo huo, na kikubwa wameahidi kupambana kusaka
matokeo mazuri katika mchezo dhidi ya Misri.
“Katika mpira hakuna kinachoshindikana, sie
tumejiandaa vizuri, naamini tutakapofika Misri tutafanya vizuri na kuwapa
furaha watanzania, kikubwa watuombee kwa mwenyezi mungu, tuwe wazima mpaka siku
ya mchezo, naamini tutafanya vizuri” alisema Nadri.
Stars inatarajiwa kuelekea jijini Cairo siku ya
ijumaa, kisha kuunganisha katika jiji la Alexandria tayari kwa mchezo dhidi ya
Misri utakaochezwa katika uwanja wa Boeg El Arab siku ya jumapili Juni 14,
2015.
0 COMMENTS:
Post a Comment