KOCHA WA SIMBA, DYLAN KERR, RAIA WA UINGEREZA ANAYETARAJIA KUANZA KAZI JUMATATU IJAYO. |
Timu ya Simba imeingia makubaliano ya mkataba wa
mwaka mmoja na kocha raia wa Uingereza, Dylan Kerr ya kukinoa kikosi hicho
kwenye msimu ujao wa Ligi Kuu Bara.
Rais wa timu hiyo, Evans Aveva alisema kuwa kocha
huyo anatarajiwa kutua nchini wiki hii tayari kwa kuanza kibarua cha kukinoa
kikosi hicho.
Avea alisema, kocha huyo mara ya kutua nchini
atazungumza na Waandishi wa habari na Jumatatu ya wiki ijayo ataanza kibarua
rasmi cha kukinoa kikosi hicho chini ya kocha msaidizi, Selemani Matola.
“Tumeingia makubaliano mazuri na kocha wetu mpya,
Kerr tayari kwa kuanza kibarua cha kukinos chetu kwenye msimu ujao, hiyo ni
baada ya kufikia muafaka kabla ya kusaini mkataba wa mwaka mmoja.
“Kocha huyo anatarajiwa kutua nchini wiki hii na
Jumatatu ijayo ataanza mazoezi ya pamoja ya kuifundisha timu yetu tayari kwa ajili
ya kuanza msimu mpya wa ligi kuu.
“Pia ningependa kumtangaza kocha wetu mpya wa
makipa mpya raia wa Kenya, Abdul Idd Salim ambaye ataanza kibarua cha kukinoa
kikosi hichi,”alisema Aveva.
0 COMMENTS:
Post a Comment