Simba imeamua kufanya mambo yake kimyakimya
na kufanikiwa kunasa mshambuliaji Mrundi, Laudit Mavugo.
Habari za uhakika zimeeleza, Simba
imemsajili Mavugo kwa mkataba wa miaka miwili na mjumbe wa kamati ya utendaji,
Collins Frisch ndiye alifanya kazi hiyo mjini Bujumbura, wiki iliyopita.
“Kweli alikuja hapa yule ofisa wa Simba,
wamemalizana na Mavugo na kila kitu kimekwenda sawa,” kilieleza chanzo kutoka
Bujumbura.
Hata hivyo imekuwa ikielezwa kwamba Mavugo ana mkataba binafsi na bosi wa timu yake ya Vital'O jambo ambalo Simba lazima walimalize kabla ya kupata uhamisho.
Simba ilikuwa ikishindwa kufanikisha dili
hilo kwa straika huyo aliyekuwa akikipiga katika timu ya Vital’O baada ya
kuibuka kwa machafuko ya kisiasa yaliyoenea nchini Burundi kutokana na baadhi
ya raia wa nchi hiyo kupinga kitendo cha Rais Pierre Nkurunziza kuwania nafasi
hiyo kwa awamu ya nne.
Wiki iliyopita, Mwenyekiti wa Kamati ya
Ufundi ya Simba, Collin Frisch alitinga Burundi kwa ajili ya kwenda kujua mbivu
na mbichi juu ya hatma ya kumtia mikononi mchezaji huyo na hatimaye akarejea na
jibu zuri.
0 COMMENTS:
Post a Comment