Timu ya soka ya Mwadui ya mkoani Shinyanga iliyopanda daraja hivi
karibuni, imeionyesha Yanga kuwa nayo ipo vizuri kifedha na inaweza kushindana
nayo katika vita ya usajili ambayo inazidi kushika kasi hapa nchini.
Pamoja na Luhende, Mwadui FC ilimsajili kiungo mkongwe, Nizar Khalfan kutoka Yanga.
Ijumaa iliyopita Mwadui FC ilifanikiwa kumsajili aliyekuwa beki wa
kushoto wa Mtibwa Sugar, David Luhende ambaye pia alikuwa akiwaniwa na mabingwa
wa Ligi Kuu Bara, Yanga, waliokuwa wakitaka kumrudisha kundini ili waweze
kuongezea nguvu kwenye safu yao ya ulinzi.
Inadaiwa kuwa Yanga ilikuwa imemtengea Luhende kitita cha shilingi
milioni 8 ili iweze kuipata saini yake lakini Mwadau FC iliingilia kati na
kuweza kuipiku klabu hiyo baada ya kumwekea mezani nyota huyo Sh milioni 10.
“Tunamshukuru Mungu ndugu yetu kapata timu ambayo imeonyesha
kumjali na kuithamini kazi yake baada ya Mwadui kuamua kumpatia mkataba wa
mwaka mmoja kwa kitita cha Sh milioni 10 lakini pia atakuwa akilipwa mshahara
wa shilingi milioni moja kwa mwezi.
“Uamuzi huo wa Mwadui tumeupokea kwa mikono miwili na imeonyesha
kuwa, wapo vizuri kifedha kwani wameweza kuipiku Yanga ambayo pia ilikuwa na
nia ya kutaka kumrudisha kundini ila kiasi cha fedha walichokuwa wamemtengea
kilikuwa ni kidogo sana,” kilisema chanzo hicho cha habari.
Hata hivyo, Luhende amesema kuwa anajiona ni mwenye
bahati na atahakikisha anaitumikia klabu hiyo kwa nguvu zake zote kwa sababu
soka ndiyo kazi yake inayomfanya aishi vizuri na familia yake.
0 COMMENTS:
Post a Comment