Kocha Mkuu wa
Togo, Tom Saintfiet amecharuka kuhusiana na nyota wake, Emmanuel Adebayor kuchelewa
kujiunga na wenzake.
Saintfiet aliyewahi
kuinoa Yanga na kuipa ubingwa wa Kombe la Kagame amesema Adebayor ameonyesha
utovu wa nidhamu.
Kocha huyo raia
wa Ubelgiji amesema, Adebayor ameonekana siku mbili tofauti lakini hakwenda
kambini kuungana na wenzake wanaojiandaa kuipigania Togo kufuzu Kombe la
Mataifa Afrika.
“Kweli ni
mchezaji muhimu, lakini si sahihi alichofanya na siwezi kufanya kazi na mtu
asiyejali nidhamu.
“Tunapokuwa
katiaka kikosi, basi kila mchezaji anakuwa sawa na mwingine, hakuna anayewazidi
wengine hata kama atakuwa muhimu zaidi ya wengine,” alisema kocha huyo mkali
katika suala la nidhamu tokea akiwa Yanga.
Togo inashuka
dimbani nyumbani dimbani jijini Lome, Jumapili dhidi ya Liberia kufuzu kucheza
Kombe la Mataifa Afrika.
0 COMMENTS:
Post a Comment