Timu ya soka ya taifa
ya Tanzania,Taifa Stars inayodhamini na kampuni ya bia ya Kilimanjaro, leo
imeanza mazoezi katika Uwanja wa Addis Ababa zamani ukifahamka kama
(Haille Sellsie) uliopo jijini Addis Ababa kujiandaa na mchezo dhidi ya Misri
utakaopigwa Juni 14, jijini Alexandria.
Stars ambayo
iliwasili jana jioni jijini Addis Ababa imefikia katika hoteli ya Debre Damo
iliyopo eneo na 22 Mazoiria ambapo itakaa kambi kwa kipindi cha wiki moja
kujiandaa na mchezo dhidi ya Mafarao.
Kocha Mkuu wa
timu ya Taifa Stars Mart Nooij amesema anashukuru vijana wake wamefika salama,
na wapo katika hali nzuri, anaamini wiki moja ya maandalizi nchini Ethiopia
itasaidia kikosi chake kuwa fiti ajili ya mchezo.
Akiongelea
kuhusu kambi, kocha Nooij amesema kwa kuwa mji wa Addis Ababa upo katika ukanda
wa juu( mita 2000 kutoka usawa wa bahari), kambi ya mazoezi itakua nzuri
kutokana na wachezaji kufanya mazoezi katika hali hiyo na kwenda kucheza katika
ukanda wa kawaida.
Kuhusu hali
ya hewa ni nzuri kwani baridi iliyopo kwa sasa Addis Ababa ni ya kawaida, hivyo
haitaweza kuwasumbua wachezaji katika maandalizi ya mchezo dhidi ya Misri.
Mchezo kati
ya Misri na Tanzania unatarajiwa kuchezwa katika jiji la Alexandria ambalo lipo
eneo la bahari ya Mediteranian.
0 COMMENTS:
Post a Comment