Straika mkongwe anayerejea kuichezea Simba, Mussa Mgosi, amesema
kwa namna yoyote ile, ni lazima avae jezi namba 11 klabuni hapo ambayo
inavaliwa na Ramadhan Singano ‘Messi’.
Mazungumzo ya Mgosi na Simba kuhusu kujiunga na timu hiyo yapo
katika hatua nzuri na muda wowote atasaini mkataba wa kuichezea timu hiyo
akitokea Mtibwa Sugar.
Mgosi aliliambia Championi Jumamosi kuwa, mara zote anapokuwa
katika timu anayochezea hata kwenye ‘ndondo’, hupenda kuvaa jezi namba 11
akiamini ina mafanikio kwake.
“Siwezi kuzungumza mengi kuhusu Simba kwani tupo katika hatua nzuri
na nina imani nitakuwa nao msimu ujao, kuhusu jezi mimi napenda kuvaa namba 11
na ndiyo nitakayoivaa Simba,” alisema Mgosi ambaye amemaliza mkataba na Mtibwa.
Hata hivyo, Mgosi anaweza akajichukulia kiulaini jezi hiyo namba
11 kwani Messi kwa sasa yupo katika malumbano na uongozi wa Simba kuhusu muda
wa mkataba wake kwani mwenyewe anasema umeisha huku uongozi ukisema bado ana
mwaka mmoja zaidi.
0 COMMENTS:
Post a Comment