Kikosi cha Azam Fc kitakachoshiriki michuano ya Kagame, kinaarajia
kuweka kambi mjini Tanga.
Chini ya Muingereza, Stewart Hall kinatarajia kuondoka siku yoyote
ndani ya wiki hii kwenda kuweka kambi.
Azam FC ikiwa mjini humo, itapata nafasi ya kucheza mechi za
kirafiki kujipima nguvu shisi ya wakongwe African Sports na Coastal Union.
Msemaji wa timu hiyo, Jaffar Idd Maganga, alisema wanaenda kuweka
kambi mkoani humo kutokana na maagizo maalumu ya kocha wao ya kutaka kwenda
kuweka kambi nje ya Dar.
“Ni kweli kuwa tunaenda kuweka kambi maalumu mkoani Tanga kwa
ajili ya kujiweka sawa kabla ya kuanza kwa ligi kuu pamoja na mashindano ya
Kagame.
“Kambi hii ni maalumu kutokana na maagizo ya kocha Stewart Hall
pamoja na benchi lake la ufundi kuhitaji timu kwenda kuweka kambi nje ya jiji
la Dar ambapo tukiwa mkoani humo tutacheza michezo ya kirafiki na timu za
Coastal na African Sports kwa ajili ya kupima ubora wa kikosi chetu,” alisema
Maganga.
0 COMMENTS:
Post a Comment